Takribani wagonjwa 17 wameripotiwa kufariki baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuliko katika hospitali ya mji wa Tula,Mexico.
Baadhi ya wahanga walikuwa hospitali hapo wakipatiwa matibabu ya uviko 19 kwa kutumia mashine ya oxygen, kabla ya kingo za mto kupasuka, maji kusambaa na kusababisha umeme kukatika.
Wagonjwa arobaini ( 40 ) wamefanikiwa kuhamishwa na kikosi cha uokoaji wakati boti iliyokuwa ikimsafirisha Gavana wa Jimbo hilo Omar Fayad Ilizama ingawa hakupata madhara na hali yake ni salama kama alivyoeleza kupitia mtandao wa twitter huku akisisitiza kwamba mamlaka za serikali zitaendelea kuratibu shughuli za dharura na uokoaji katika maeneo yaliyoathirika.
Naye Rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador amesema amesikitishwa sana na vifo vilivyotokea hospitali hapo.
amewataka wakaazi wa maeneo yaliyoathirika kuhama makazi hayo au kukaa na jamaa na marafiki katika maeneo salama.
Zaidi ya watu 30,000 katika miji mbalimbali nchini humo wameathiriwa na mafuriko hayo.