Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Dorothy Gwajima amesema kuanzia leo July 22,2021 amepiga marufuku shughuli zote za misongamano yote isiyo ya lazima na ile yenye ulazima tahadhari ya kutosha ichukuliwe bila kuathiri shughuli za kiuchumi na Kitaifa.
‘ili kuimarisha zaidi kasi ya kupambana na kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19 natamka kuwa, kuanzia leo tarehe 22/07/2021 nimekataza shughuli zote za misongamano yote isiyo ya lazima na ile yenye ulazima tahadhari ya kutosha ichukuliwe bila kuathiri shughuli za kiuchumi na kitaifa’- Waziri wa Afya
‘Naelekeza Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuwapa ushirikiano Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria ya Afya ya Jamii Na. 1 ya Mwaka 2009 na kuweka utaratibu mzuri kwa wale wanaoomba vibali vya shughuli zenye ulazima’- Waziri wa Afya
‘Natoa wito kwa wananchi wote kujiandaa kupata huduma ya Chanjo kama ambavyo Mheshimiwa Waziri Mkuu alivyotoa taarifa jana tarehe 21/07/2021’- Waziri wa Afya
Leo hii wataalamu wa afya wamekutana kupata mafunzo tayari kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma ya Chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa hiari na bila malipo’-Waziri wa Afya
‘Idadi ya wagonjwa wanaougua maradhi ya UVIKO-19 Tanzania imeongezeka na kufikia 682′-Waziri wa Afya