Top Stories

Wagonjwa wapya wa Corona Kenya 134 jumla 2474

on

Katibu wa Wizara ya Afya Mercy Mwangangi ametangaza Ijumaa kuwa idadi ya waliothibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19 nchini Kenya imeongezeka na kufikia 2,474.

Akitoa taarifa ya kila ya siku kutoka kwa wizara kuhusu maambukizi mapya, Dkt. Mwangangi amesema watu 3,177 wamepimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita huku 134 wakithibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Wizara hiyo imeongeza kwamba watu 90, 875 wamefanyiwa vipimo nchini Kenya hadi kufikia Juni 5.

“CORONA IMEISHA TUTAFUNGUA SHULE ZA MSINGI NA CHEKECHEA HIVI KARIBU” RAIS MAGUFULI

Soma na hizi

Tupia Comments