Top Stories

Wahamiaji haramu 61 wakamatwa wakisafirishwa kwenye lori (+video)

on

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya, limewanasa wahamiaji haramu 61 raia wa Ethiopia wakiwa wanasafirishwa kwenda nchi jirani ya Malawi kwa kutumia lori la mizigo huku dereva wa gari hilo pia akishikiliwa kwa kosa la kusafirisha wahamiaji hao.

Akizungumza na wandishi wa habari katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Mbeya, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Jerome Ngowi, amesema wahamiaji hao walikamatwa juzi katika kizuizi cha magari kilichopo kijiji cha Gari Jembe barabara Kuu ya Tanzania na Malawi.

Amesema wahamiaji haramu hao walikuwa wamefichwa kwenye lori aina ya Scania yenye namba za usajili T. 509 AZZ ambalo lilikuwa linaendeshwa na dereva ajulikanaye kwa jina la Rabdi Ramadhani (48) mkazi wa Unga Limited mkoani Arusha.

MAPYA YA ‘MGANGA’ WA SIMBA “ANGEFUNGA ANGEKUFA, NINA PAKA 40, BILA UCHAWI HAWASHINDI”

 

Soma na hizi

Tupia Comments