Wahisani waliahidi jumla ya dola bilioni 2.4 Jumatano, zikiwemo ahadi mpya zatakriban dola bilioni moja kwa ajili ya Pembe ya Afrika iliyokumbwa na ukame wakati wa mkutano wa wafadhili uliofanyika katika makao makuu ya UN, lakini wakashindwa kufikia lengo la dola bilioni 7 zinazohitajika.
Katibu mkuu wa UN, Antonio Guterres, amesema watu zaidi ya milioni 32 kwenye mataifa ya Kenya, Somali na Ethiopia, wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu kunusuru maisha yao.
Hata hivyo licha ya hatua hii, lengo la awali la kupata dola bilioni 7 halikufanikiwa, mashirika ya misaada yakitoa wito wa kupatikana kiasi hicho cha fedha kwa wakati.
Hatua hii inakuja wakati huu zaidi ya watu milioni moja nchini somali katika kipindi cha miezi minne wakiwa hawana malazi katika nchi yao wenyewe, kutokana na madhila kadhaa ikiwemo ukame, vurugu na mafuriko, imesema taarifa ya mashirika ya misaada ya kibinadamu.
Kulingana na shirika linalowashughulikia wakimbizi na baraza la wakimbizi la Norway, watu laki 4 na elfu 33, walilazimika kuhama nyumba zao kati ya Januari Mei 10, wakati ghasia za wanajihadi wa kiislamu zilipozuka katika eneo lililojitenga la Somalilanda.