Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewapongeza wahitimu bora wa Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) cha Morogoro kwakuwapatia zawadi ya fedha taslimu shilingi milioniTano (5)
Motisha hiyo ya fedha, imetolewa na TADB kamasehemu ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizurizaidi kupitia mpango mkakati wake mpyauliozinduliwa mwaka huu.
Akiongea wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwawanafunzi waliofanya vizuri na wafanyakazi katikaeneo la utafiti, Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa TADB Bi. Jacqueline Minja alisema hatua hiyo ni sehemu yakuunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa naMhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Benki yetu inatambua uwepo wa mikakati mbalimbaliya serikali kama vile sera ya Taifa ya Maendeleo yaVijana ya mwaka 2007 ambayo imetilia mkazoumuhimu wa kuweka mazingiza wezeshi kwa vijanakujihusisha na shughuli za kiuchumi, ikiwemo kilimocha kisasa na kibiashara. Kwa kutambua hili, kwakuanza, TADB imefika hapa na kutoa tuzo kwawanafunzi bora mwaka huu.”
Afisa rasilimali huyo alieleza kuwa, katika awamunyingine, benki itaandaa programu maalumu yakuatamia vijana bora kutoka chuo kikuu cha SUA ilikutoa fursa ya kujifunza kazini.
“Programu hiyo itakayokuwa ya miezi 24, italengakutoa nafasi kwa wahitimu bora kuweza kupata nafasiya kujifunza kazi kwa vitendo katika benki yetu,” Alieleza Bi. Minja.
Akizungumza katika mahafali hayo, Kaimu Mkuu waChuo Prof Raphael Chibunda aliishukuru TADB kwakutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuripamoja na mpango wake wa kuandaa programumaalum ya kuwaatamia wahitimu wa fani ya kilimo.
TADB itaendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) katika juhudi za kutengeneza vijanawabobezi katika sekta ya kilimo ili kuwezesha vijanakuchangia kufikia malengo ya serikali ya ‘Agenda 10/30’.