AyoTV

Mbunge Mwita Waitara hajafurahishwa Waandishi kuzuiwa kurekodi chochote bungeni

on

April 19 2016 Bunge la 11 lilianza rasmi bungeni Dodoma na baadhi ya Wizara zilianza kwa kuwasilisha bajeti zake na kutoa nafasi kwa washiriki kuzikubali au kuzikataa lakini ishu moja ambayo imekwaza hasa Wabunge wa upinzani ni kuzuiwa kwa matangazo ya bunge kuonyeshwa live kwenye bunge na Waandishi wa habari kuzuiwa kurekodi chochote ndani ya bunge.

Utaratibu mpya ni kwamba kuna timu maalum iliyopewa kazi maalum ya kurekodi matukio yote yanayofaa kufikishiwa Wananchi na hayo matukio ndio wanapewa Waandishi wa habari ila hakuna tena utaratibu kama wa zamani kwamba kila mwandishi anaweza kurekodi kwa Camera yake chochote anachoona ni habari.

Hapa nakukutanisha na Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara anaesema >>> ‘Kabla ya kuja bungeni tuliona taarifa ya kuwa TBChaitaonyesha vipindi vyote tena bali itaonyesha live kipindi cha maswali na majibu tu pale asubuhi lakini sehemu nyingine ya matangazo ya bunge itarekodiwa na kitengo maalum kisha Waandishi kupewa material’

Vyombo binafsi vya habari vinaweza kutoa taarifa kwa gharama zao lakini vimezuiwa kurusha bunge live , kitendo kilichofanyika ni kuwazuia waandishi, huu ni uoga wa Serikali na ni kuwaondoa watu katika utandawazi, TBC iliposema haina pesa ya kurusha LIVE kuna vyombo vya habari binafsi vimesema vinauwezo wa kurusha ila navyo vimezuiwa‘ – Mwita Waitara

Kwenye sentensi nyingine Mwita Waitara amesemaWaziri Nape Nnauye alisema vyombo binafsi vingeruhusiwa kurusha live matangazo ya bunge baada ya TBC kuona ni gharama kubwa kurusha live ni bora pesa zipelekwe kusaidia Wananchi, kitendo kilichofanyika ni kibaya tangu tumepata uhuru…. leo bunge linaendeshwa watu wapo gizani, kama wanatoza Wananchi kodi mtaani kwanini wanyime Wananchi kuona pesa zao zinapangwa vipi kwenye bajeti? wanazuia Watanzania wasipate taarifa ili wawadanganye

Mtazame Mwita Waitara kwenye hii video hapa chini…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Ilikupita hii Video ya Diamond Platnumz, Mrisho Mpoto Walivyotajwa Bungeni?

 

Soma na hizi

Tupia Comments