Mkuu wa mkoa Morogoro Adam Malima amesema serikali itaendelea kulinda na kutetea haki za wajane Ili waendele kulea familia zao.
Rc Malima ameyasema hayo Mjini Morogoro kwenye maadhimisho ya Siku ya wajane Duniani ambapo kitaifa yameadhimishwa Mkoani Morogoro ambapo amesema kumekua na tabia ya baadhi ya watu kuchukua Mali pamoja na kuwafukuza wanawake kinguvu baada ya kufiwa na waume zao hivyo serikali haitavumilia jambo hilo.
Aidha Rc Malima amewataka wajane kuwa pamoja katika kutetea hako zao na kutofumbia macho ukatili wanaofanyiwa katika Jamii zao zinawazo wazunguka.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha wajane Tanzania(CCWWT) Sabrina Tenganamba amesema moja ya Changamoto inayowakabili ni ukosefu wa Elimu ya sheria kwa wajane hasa vijijini.
Sabrina ameomba serikali kuwawezesha wajane kupata mikopo isiyo na riba Kwani Kwa Sasa wanakumbana na Changamoto ya mikopo umiza ambayo imekua Changamoto kwao kujikwamua kiuchumi na kuendelea kuwa tengemezi
Naye Nashori Miloki mjane Jamii ya kimaasai anasema mila na desturi wa kabila hilo zimekua kandamizi kwani wanawake hawaruhusiwa kumiliki ardhi hivyo Jitihada inahitajika katika utoaji Elimu.
Naye Mwakilishi wa Kituo cha msaada wa kisheria Morogoro (MPLC) Peter Kimath ametoa wito kwa Jamii kushirikiana na kituo hicho katika msuala ya Sheria.