Hii video inaonesha baadhi ya Watu wakiwemo Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Perm wakijirusha kutoka gorofani ili kuokoa maisha yao baada ya Mwanachuo mwenye bunduki kuingia chuoni akiwa na Bunduki na kuanza kuua Watu ovyo ambapo taarifa zimesema hadi sasa ni Watu wanane wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa.
Kamati ya Upelelezi ya Urusi ambayo inachunguza matukio makubwa ya kihalifu imesema Mshambuliaji huyo ameuawa, taarifa za awali zinasema Mshambuliaji huyo ni Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18 na Jina lake ni Timur Bekmansurov, bado haijajulikana kwanini amefanya mauaji hayo.
PROFESSOR JAY KAIBUKA KWENYE AFTER PARTY YA SIMBA SC, KAWAIMBISHA MWANZO MWISHO