Wakala wa mchezajiwa Liverpool Mo Salah anayejulikana kwa jina la Rammy Abbas Issa amekanusha taarifa za Salah kuwa sehemu ya kikosi cha Misri U-23 kitakachoshiriki michuano ya Olympic nchini Japan.
Mapema leo zilitoka taarifa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Misri U-23 Shawky Gharib anakusudia kumjumuisha mchezaji huyo katika list ya wachezaji watatu waliozaidi ya umri wa miaka 23 katika kikosi hicho.
Rammy amesema kuwa Salah ,27, bado hajafanya maamuzi na hakuna mazungumzo yaliofanyika na kudaiwa kuwa hawezi kuitwa mchezaji kwa meseji “Hapana uamuzi bado haujafanyika”, Salah bado hajaongea na Shawky na endapo atakubali atakosa Pre Season akiwa na Liverpool.
Michuano ya soka ya Olympic kwa kawaida inashirikisha timu za taifa zenye umri chini ya miaka 23 lakini kila nchi shiriki wanaruhusiwa kuongeza wachezaji watatu walio zaidi ya miaka 23 kama watapenda kufanya hivyo.