Habari za Mastaa

Wakazi awachana wasanii na video directors wanaochukulia Poa Corona

on

Msanii wa Hip Hop Bongo, Wakazi ameshindwa kuvumilia kuona baadhi ya wasanii na video’s Director wanaochukulia Poa swala la ugonjwa wa Corona kwa kuendelea na shughuli zao ambazo zinahusika moja kwa moja kukusanya watu.

Wakazi amewachana kupitia Instagram page yake na kuwaeleza kuwa hata wao wana njaa ya kutaka kufanikiwa ila wameamua kuacha shughuli zao za kimuziki na kuelimisha Kwanza watu kuhusu Corona.

Wakazi ameandika…>>>“Stop being Covidiots !!! Wote tuna njaa ya Mafanikio, ila usalama wa Afya ni Kipaumbele. Ukishindwa kusimamisha shughuli za uzalishaji, basi atleast weka mazingira ambayo yanaonyesha kuwa unajali na kuzingatia.

“Maji na Sabuni AU sanitizer kwenye video sets, kupunguza scripts zinazohusisha kushikana shikana sana (practice Social Distancing). Directors, Artists, Makeup Artists, Stylists, Set Guys & Models be responsible.” – Wakazi

VIDEO: MAHABA YA TID KWA LULU DIVA AMWIMBIA LIVE 

Soma na hizi

Tupia Comments