Katika mitandao ya kijamii, Wakenya wanaendesha kampeni maalumu huku wakihimizana kujaza fomu ya mahakama ya Kimataifa ya jinai, ICC, kwa ajili ya kuishitaki serikali ya Rais William Ruto.’
“Chini ya Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka (“OTP”) inaweza kuchambua taarifa kuhusu uhalifu unaodaiwa ndani ya mamlaka ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, mauaji ya halaiki na uchokozi), iliyowasilishwa kwake. kutoka kwa chanzo chochote,” fomu hiyo inasema.
Kampeni hii inakuja huku kukiwa na matukio ya utekaji nchini Kenya. Wiki iliyopita, vijana saba waliotekwa Disemba 2024 waliachiliwa.
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai imezingatia malalamiko kadhaa ikiwemo
Uhalifu wa kivita ambao ni pamoja na mateso, utekaji, adhabu ya viboko na vitendo vya kigaidi vinaweza kushitakiwa katika Mahakama ya ICC.
Makosa ya jinai ikiwa ni kesi inayojumuisha vitendo vyote vinavyofanywa kwa nia ya kuharibu kikundi cha kitaifa, kabila au dini.
Uhalifu dhidi ya ubinadamu ikiwa ni vitendo vinavyofanywa kama sehemu ya shambulio lililoenea au la kimfumo dhidi ya raia wowote, kama vile mauaji, kuhamisha watu kutoka makazi yao, mateso na ubakaji.