Wakulima wa zao la tumbaku wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kuweka uchafu kwenye zao hilo wakati wa kuingiza sokoni kwani jambo hilo linaweza kusababisha wanunuzi kushindwa kununua tumbaku ya nchini na kukosa soko la kimataifa
Wito huo umetolewa na Collin Nyakunga ambaye ni Naibu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Katika mkutano mkuu wa tano wa mwaka wa chama cha ushirika cha TCJE mjini Morogoro ,naibu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini kutoka tume ya maendeleo ya ushirika anasema hujuma hizo kamwe hazikubaliki nakusema tume inaendelea kufuatilia kwa karibu sana wakulima wa zao la tumbaku nchini.
Wanunuzi nao wamekuwa wakitumia kigezo cha ubora wa tumbaku katika kufanya uamuzi wa kununua tumbaku katika soko lakini inaelezwa kuwa uwaminifu umekuwa mdogo mno kwa baadhi ya wakulima.
Nyakunga anasema Tumbaku ya Tanzania ni zao ambalo linakubalika katika soko la kimataifa hivyo hali hiyo inajenga picha mbaya na kuharibu taswira ya nchi kwenye zao hilo
Aidha wakulima hao wametakiwa kuepuka migogoro kwenye vyama vya ushirika ambayo inaweza kurudisha nyuma maendeleo ya ushirika na mkulima mmoja mmoja
Kwa upande wake mkurugenzi Mkurugenzi Bodi Tumbaku Stanley Mnozya amesema kwa sasa hali ya uzalishaji tumbaku imeongezeka nchini kutoka tani milioni sitini hadi tani milioni mia moja huku lengo kufika tani milioni mia mbili ifikapo 2025
Anasema pamoja na hayo pia wanunuzi wa zao hilo wameendelea kuongezeka jambo ambalo linaleta tija kwa wakulima kuongeza uzalishaji zaidi.