Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imewataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuwa sehemu ya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya kilimo kama wanavyo heshimu maandalizi ya mbio za mwenge ili kuleta mapinduzi ya kilimo ambacho ni kutega uchumi na kiinua mgongo cha watanzania.
Bashe amesema hayo katika hafla ya utiaji saini ya makubaliano na wakurugenzi wa Halmashauri 19 nchini juu ya usimamizi,uendeshaji na matunzo ya skimu za umwagiliaji kati ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Vyama vya Umwagiliaji kupitia miradi ya mifumo himilivu ya chakula Tanzania.
“Hii Nchi nimewahi kuwa na mifumo ya Umwagiliaji huko nyuma ikafa kwasababu hakukuwa na usimamizi kwenye ngazi ya Halmashauri lazima tutengeneze ‘bond’ kwamba mtu wa umwagiliaji aliyepo kwenye wilaya mnapokaa kupanga maendeleo apewe nafasi lazima pia mkurugenzi wa Halmashauri ujue kazi anazozifanya” Hussein Bashe
“Siku tukiheshimu Kilimo Cha Nchi hii kama tunavyoheshimu mwenge tutaondoa umasikini wa watu sana na hiki kikao ni mwanzo mpya kati ya wakurugenzi na Wizara ya Kilimo na nawambie hii Nchi yetu tatizo sio wakulima mimi niaka saba serikalini sasa tatizo ni sisi” Bashe Waziri wa Kilimo