Chama Cha Wakutubi Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa habari wameshauri kuja na mwongozo wa maadili ya teknokojia ya habari na mawasiliano ambao utaweza kutumika Kwenye maktaba pamoja na vituo vya habari nchini.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Omar Mgumba wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa 49 wa mwaka wa Chama Cha Wakutubi Tanzania TLA unaofanyika mkoani Tanga.
Alisema kuwa kutokana na maendeleo ya teknolojia ya habari kwa Sasa hapa nchini na duniani Kwa ujumla mwongozo huo utaweza kusaidia kutatua changamoto za kimtandao zinazojitojeza Kwa Sasa ambazo zinachangia ukosefu wa maadili Kwa wananchi.
“Maendeleo ya kiuchumi yanategemea upatikanaji wa taarifa na habari Kwa usahihi hivyo kutokana na kutokuwa na mwongozo kumekuwa na upotoshaji mkubwa ambao unaendeleaje huko kwenye mitandao”alisema RC Mgumba.
Nae Mwenyekiti wa chama Cha Wakutubi Tanzania TLA Prof Ali Mcharazo alisema kuwa Ili maktaba zetu na watoa huduma waendane na Kasi ya utendajikazi wameanza kutoa elimu ya tehama Kwa wanachama wao.
Alisema kuwa elimu hiyo itaweza kusaidia kwenda sambamba na mabadiliko ya utoaji wa huduma za maktaba Kwa njia ya mtandao na hivyo kusogeza huduma Kwa wananchi.