Mkuu wa mkoa wa tanga Waziri Kindamba amewataka wakuu wa wilaya wote na wakala wa misiti TFS mkoani Tanga kutokutoa vibali vya ukataji wamiti kwenye maeneo yao.
Kindamba ameyasema hayo katika kampeni maalumu ya upandaji wa miti iliyo ratibiwa na shirika la World Vision chini ya mradi wa sauti iliyofanyika mkoani hapa nan a kuhusisha maandanao ya Amani ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira na upandaji miti kwa viongozi mbalimbali wa serikali na sekta binafsi,ambapo amesema kuwa lengo la serikali ni kupanda miti isiyopungua milioni moja laki tano kila
mwaka .
“sisi tunakampeni ya kupanda miti hivyo niwatake ndugu zangu wa TFS kuongeza kuvu ya kupanda miti kwanza vibali vya kukatakata miti mwisho kutoa sisi tuna kampeni ya kupanda miti nasio kukata miti anaye taka kukata miti tutamkata yeye hakuna kukata miti hapa Tanga”Alisema kindamba.
Kwaupande wake Mkurugenzi anayesimamia maswala ya mahusiano na serikali la World Vision Tanzania Dr.Joseph Myala alisema kuwa kampeni hiyo ni utekelezaji wa mpangi mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa mwaka 2021 hadi 2025 ambapo amebainisha kuwa upo mpango kwa kufanya mradi mwingine utakao shirikisha serikali pamoja na wananchi .
Hata hivyo miti takribani 300 imepandwa katika shule ya msingi ya usagara huku wito ukitolewa kwa wananfunzi kuendelea kuitunza miti hiyo .