Naibu Waziri Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde alikuwa mgeni rasmi katika utoaji wa fimbo za kisasa 30 zilizotolewa na kampuni ya Next Generation Microfinance zanye thamani ya Shilingi Mil 1.8 kwa ajili ya kuwasaidia watu wasioona mkoani Dodoma ikiwa ni kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku.
“Niwashukuru sana kampuni ya Next Generation kwa kuamua kutoa sehemu ya faida yenu kwa ajili ya kundi hili lenye mahitaji makubwa katika jamii, Walemavu wanahitaji sana upendo na ukaribu wetu kila siku”-Anthony Mavunde
“Mmesema mnafanya haya ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli, hili ni fundisho kwetu kwa kila mmoja kuona namna anavyoweza kutoa misaada bila kutegemea kila kitu kufanywa na Serikali. Mngeweza mkaamua kufanya sherehe yenu wenyewe ya mwisho wa mwaka lakini mkaona bora kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum”-Anthony Mavunde
Full video nimekuwekea hapa chini tayari….