Wadau wa Sekta ya Michezo nchini wameombwa kuziangalia timu za watu wenye Ulemavu kwani zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa Ligi za ndani.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam wakati timu ya watu wenye Ulemavu nchini ilipopokea msaada kutoka Taasisi ya Nifuate ambayo imejitolea kuiunga mkono Timu hiyo ya Tanzania kuelekea mchezo wao dhidi ya Mombasa, April 28,2023.
Ibrahim Mbarouk Saleh ambaye ni Mkurugenzi wa Nifuate Foundation amesema—“Taasisi imejitolea kuisaidia timu ya Walemavu ambapo imewadhamini mechi ambayo inatarajiwa kuchezwa hivi karibuni,”
“Tunaomba wadau wajiyokeze katika jambo hili, kikubwa tunaweza kusema timu za walemavu zimesahaulika sana, pia tunaiomna serikali iwatazame wenye vipaji vya mpira,”.
Bashra Hassan Alombile ambaye ni mmoja wa wachezaji katika timu hiyo amesema kuwa…..“Tunawapongeza Nifuate Foundation na watu wachache wenye moyo kama huu kuangalia jamii ya watu wenye ulemavu ikizingatiwa kwamba tunaonekana kama watu omba omba lakini wameangalia kupitia huu mchezo wetu wa miguu wameona wanaweza kutengeneza kitu ili tuweze kusaidia familia zetu,”amesema.
“Kwa upande wetu wachezaji hatuna ligi kwani ukiangalia tunajiandaa dhidi ya mchezo wetu na Mombasa lakini baada ya mchezo huu hatuna mechi nyingine,”- Amesema