Watu wawili ambao wametoka gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais Samia Suluhu wameuawa na Wanachi wenye hasira kali baada ya kukamatwa wakidaiwa kuiba vitu mbalimbali Kibaha mkoani Pwani.
Watu hao ni Ramadhani Mohamedi maarufu Seven au Ali (28) na Idd Hamisi maarufu Chuga (30) wote wakazi wa Kibaha na walifungwa kwa makosa ya wizi kabla ya kupata msamaha wa Rais Aprili 12 mwaka huu kutoka katika gereza la Mkuza lililopo Kibaha.
RPC wa Pwani Wankyo Nyigesa ametoa taarifa leo May 10, 2021 na kusema Watu hao wameuawa juzi May 08,2021 kwa kupigwa na mawe, mapanga na fimbo wakituhumiwa kuiba.
“Niwasihi Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha hasira na badala yake watoe taarifa Polisi inapotokea tukio la wizi kwenye maeneo yao, ili watuhumiwa wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria” RPC Pwani