Top Stories

Waliofariki baada ya kugongwa na Mwendokasi watajwa, kamanda atoa onyo (video+)

on

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lianasikitika kutoa taarifa ya ajali iliyohusisha basi la Mwendokasi na Pikipiki iliyopelekea vifo vya watu wawili.

Ajali hiyo ilitokea tarehe 08/09/2021 majira ya saa 21:20 usiku katika barabara ya mwendokasi eneo la Lumumba kwenye taa za kuongozea magari,ambapo pikipiki yenye namba za usajili MC 663 CDX aina ya Boxer ikiendeshwa na Sami Riyaz Khan(17),Mkazi wa Gerezani, akiwa na abiria wake Patrick Chohan(16) iligongana na basi la mwendokasi lenye namba za usaji T 880 DGV aina ya Golden Dragon lililokuwa likitokea Kimara kuelekea Kivukoni na kusababisha vifo vya dereva wa pikipiki na abiria.

CCTV CAMERA ILIVYOINASA AJALI YA MWENDOKASI NA BODABODA, “WAWILI WAFARIKI PAPO HAPO” DSM

Soma na hizi

Tupia Comments