Taarifa kutoka kwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu “Wizara inatoa taarifa juu ya uwepo wa wagonjwa watano wa corona ambao wote ni Watanzania na wakazi wa DSM, aidha Waziri wa Afya Zanzibar ametangaza wagonjwa wapya wawili, hivyo waliothibitika kuwa na corona Tanzania hadi sasa ni 32 ambapo kati ya hao watano wamepona na 24 wanaendelea vizuri na matibabu”.
“Tunasikitika kutoa taarifa ya vifo viwili vilivyotokea leo miongoni mwa wagonjwa wa corona ambavyo ni Mwanaume(51) Mtanzania mkazi wa DSM na Mwanaume (57) Mtanzania Mkazi wa DSM hivyo kufanya idadi ya vifo vya corona Tanzania kufikia vitatu”-Waziri Ummy