Habari za Mastaa

Waliofariki pamoja na Kobe Bryant kwenye ajali ya Helicopter wafika 9

on

Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali ya Helicopter ambayo alikuwa amepanda marehemu Kobe Bryant imeongezeka na kufika tisa baada ya hapo awali kutangazwa kuwa waliofariki ni watano.

Kupitia kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Los Angeles kimesema kulikuwa na Watu tisa kwenye Helicopter iliyopata ajali na kusababisha kifo cha Legend wa NBA Kobe Bryant na Binti yake Gianna Bryant.

“Majina ya Watu wengine waliofariki kwenye ajali hiyo yatatolewa na Maafisa wenye Mamlaka ya kutoa taarifa hizo baada ya uchunguzi wao kukamilika na tunaomba Watu wasitoe taarifa ambazo hawana uhakika nazo tuache Mamlaka zifanye kazi yake”

Soma na hizi

Tupia Comments