Top Stories

Walioiba kofia ya Polisi, simu wafikishwa Mahakamani (+video)

on

Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni wakikabiliwa na kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha ikiwemo simu, viatu na kofia ya Polisi vikiwa na thamani ya Sh.760,500 zikiwa ni Mali ya Josephine John.

Washtakiwa ni Benny Morice (21), Mkazi wa Kiluvya gogoni na Baraka John (18) ambaye ni Mkazi wa Magomeni ambao wamesomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Frank Moshi.

Wakisomewa shtaka hilo na Mwendesha Mashtaka ASP Hamis Said, alidai washtakiwa hao walitenda kosa hilo Julai 2, 2020 eneo la Kibaha Mail Moja. Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka, Said alidai kuwa washtakiwa waliiba simu aina ya iPhone 6+ yenye thamani ya Sh.700,000, Viatu Sh.42,000, Kofia ya Polisi Sh.18,500 na muda mfupi baadae walimkata Josephine na kisu kwa nia ya kujimilikisha vitu hivyo.

Hata hivyo washtakiwa walikana kujihusisha na tuhuma hizo, wakati huo huo mwendesha mashtaka alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo anaomba tarehe nyingine.

Hakimu Moshi aliongeza kwa kusema kuwa kosa hilo alina dhamana kwa mujibu wa sheria na kesi kuhahirishwa Hadi Novemba 30, mwaka huu. Kwa upande wa Washtakiwa, wao walirudishwa rumande.

Soma na hizi

Tupia Comments