Top Stories

Waliokutwa na bangi wahukumiwa miaka 30 jela

on

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Babati, Jumaa Mwambango amewahukumu kifungo cha miaka 30 jela wakazi wawili wa wilaya hiyo baada ya kutiwa hatihani kwa kukutwa na misokoto ya bangi.

Hukumu hiyo imetolewa kwa Alex Laurent (27) na Humphley Charles (25) baada ya kukutwa na misokoto hiyo yenye uzito wa gramu 566.9.

Hukumu hiyo imetolewa bila mshtakiwa mmoja Humphrey Charles kuwepo mahakamani na tayari mahakama hiyo imetoa amri ya kutafutwa na kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo huku mwenzake akiwa ameanza kutumikia kifungo chake.

LIVE : RAIS SAMIA ANAMUAPISHA KATIBU MKUU KIONGOZI NA MAWAZIRI WATEULE IKULU CHAMWINO

Soma na hizi

Tupia Comments