Polisi nchini Hispania wamebaini kuwa kabla ya mchezo wa Madrid Derby wa Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid uliyochezwa Wanda kuna jopo la mashabikiwa wanaoaminika kuwa wa Atletico Madrid walikuwa wamejitenga kwa ajili ya kufanya vitendo vya ubaguzi wa rangi dhidi ya staa wa Real Madrid raia wa Brazil Vinicius Junior.
Vinicius ambaye alikuwa muhanga wa tukio hilo wakati wa mechi ya ugenini, polisi wamesema wamewabaini watu watano kuhusisna na tukio hilo la ubaguzi, watatu katika yao ni mashabiki wa Atletico Madrid wenye tiketi za msimu.
Matukio ya ubaguzi dhidi ya Vinicius yalianza mapema kabla, wakati na baada ya mechi, Kwa upande wa Atletico Madrid kupitia kwa CEO wao Miguel Angel Gil amethibitisha kwa kelele za nyani kusikika wakati wa mchezo lakini mashabikiwa waliohusika watafungiwa kuingia viwanjani.
AHMED ALLY ATEMA NYONGO, MJADALA WA SIMBA KUPOSTIWA CAF, EDO KUMWEMBE APIGA KIJEMBE