Top Stories

Waliomuua Mtoto na kumzika akiwa amekaa wahukumiwa kunyongwa

on

Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, imewahukumu watu wawili kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kuteka mtoto wa miaka 12 na kuwataka wazazi wake wawape fedha kiasi cha milion 5 ili wamuachie mtoto ambaye walimuuwa na kumzika akiwa amekaa huku amefungwa mikono na kichwani.

Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa  ni Tabibu Nyundo na Thobias Mtakiyicha wakazi wa Kijiji cha Gwanumpu wilaya ya Kakonko waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia kesi namba 18 ya mwaka 2021.

Imeelezwa kuwa mnamo Januari 27, 2021, washtakiwa walishirikiana kumteka mtoto huyo kisha kumtumia ujumbe wa simu jirani wa familia yake kuwa wanahitaji kiasi cha milioni 5 ili wamuachie mtoto wao .

LIVE: MAITI KUZUIWA KISA MILIONI 1.6, MUHIMBILI WAFUNGUKA “HATUDAI DENI LA MAITI, TUNADAI MATIBABU”

Soma na hizi

Tupia Comments