Top Stories

“Waliovunja kwa Polepole msako mkali watangazwa” Kamanda Dodoma

on

“Jana tarehe 12/12/2021 majira ya saa tatu na nusu katika mtaa wa Mabuba jijini Dodoma mbunge Humphrey Polepole alibaini kuvunjiwa dirisha la nyumba anayoishi na kuibiwa flat screen TV moja inch 55 na Specker moja ya Bluetooth, thamani ya mali yote hiyo bado haijaweza kufahamika” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Onesmo Lyanga

“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mbunge Humphrey Polepole umebaini alisafiri kwenda mkoa wa Manyara katika shughuli zake, upelelezi wenye kuambatana na msako mkali unaendelea ili kuwatafuta wahusika wa tukio hilo na kuwachukulia hatua za kisheria” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Onesmo Lyanga

“Suala la kwamba ni habari ya siasa sisi hatuoni kwa sababu makazi yamevunjwa kwa hiyo huwezi kusema wahalifu walikuwa wanamtafuta yeye, wangemkuta mwenyewe ishu ingekuwa tofauti ingekuwa ni unyang’anyi wa kutumia silaha au nguvu, bado haieleweki ni lini hasa palivunjwa kwa hiyo si rahisi kujua kulikuwa na nia ya kutaka kumdhuru yeye kama yeye kwa sababu hakuna ujumbe wowote ambao tumeweza kubaini kuwa umemtishia yeye maisha yake”-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Onesmo Lyanga

SHABIKI WA SIMBA ULAYA LEO ZIMEPIGWA PASI KAMA MILIONI HIVI

Soma na hizi

Tupia Comments