Mix

Coke Studio Afrika imeanza, wasanii watano wa Tanzania wamechaguliwa

on

Msimu Mpya wa Coke Studio Africa umezinduliwa rasmi Tanzania katika hafla iliyofanyika Life Park Club Mwenge Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya wageni waalikwa Mkurungezi mkuu wa Coca cola Kwanza Basil Gadzios alikiri kufurahishwa vipaji na uwezo wa wasanii watanzania watakao shiriki kwenye msimu huu mpya.

Tanzania itawasikilishwa na wasanii tano watakaotumbuiza katika msimu wa sita wa Coke Studio, wasanii hao ni Faustina Charles’ Nandy’, Raymond Mwakyusa’Rayvanny’, Rajabu Abdul’Harmonize’, Juma Jux na Mimi Mars, wasanii hao wataungana na wasanii wengine 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Kwa upande wao wasanii akiwemo Rayvanny alisema anashukuru kuwa mmoja wasanii watakaotumbuiza katika msimu huu huku akieleza hii ni mara yake ya pili.

Naye Nandy alisema kushiriki Coke studio kunakusaidia kukutana na wasanii kutoka Africa wenye vipaji lukuki…nafasi hii kwa msanii yoyote ni kitu chakujivunia sana na pia inasaidia kutengeneza kazi tofauti na kufanya jina au brand ya msanii kuimarika na nguvu katika soko la muziki Africa na dunia nzima.

Nandy alisema Coke studio ni kitu kikubwa, na hakuwahi kutegemea kukutana na msanii mkubwa kama Skales kutoka nchini Nigeria ambaye ameurdia wimbo wake wa Ninogeshe na kunuelezea kuwa ni msanii ambaye ana ushirikiano mzuri.

Soma na hizi

Tupia Comments