Takribani watoto 90 wa shule moja ya Msingi nchini Afrika Kusini wamelazwa hospitali baada ya kula Keki zinazoshukiwa kuchanganywa na bangi.
Watoto hao ambao wana umri kati ya miaka 6 hadi 14 walinunua keki hizo kwa mfanyabiashara mdogo wakiwa njiani kuelekea shuleni.
Taarifa kuhusu tukio hilo lililotokea katika mji wa Soshanguve, Kaskazini mwa Pretoria zilipatikana baada ya wanafunzi wengi kuonyesha tabia za ajabu, ndipo walimu walipopiga simu kwa Mamlaka.
Wanafunzi hao pia walipatwa na dalili zinazofanana ikiwemo kichefuchefu, maumivu ya tumbo na kutapika.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Elimu ya Gauteng Matome Chiloane ameeleza wasiwasi wake na kusema uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea.
Chiloane amewataka wazazi kuwa watulivu, na kuwaasa watoto kuwa waangalifu kwa vitu wanavyonunua , wananunua kwa nani na vitu gani