Mix

Hawa ndio wanafunzi wanaofanya mitihani ya Sekondari wakiwa na mimba.

on

Pregnant School GirlAfisa elimu katika kaunti ya Bungoma Kenya, ametoa taarifa kuhusiana na wanafunzi 53 wanaofanya mitihani wa kumaliza elimu ya sekondari iliyoanza siku ya Jumanne wiki hii, ni wajawazito.

taarifa iliyochapishwa na news 24 Kenya imesema Charles Anyika; mkurugenzi wa elimu wa kaunti hiyo amesema idadi hiyo imebainika baada ya kufanya uchunguzi, na kuongeza kuwa anategemea idadi ya wanafunzi wenye ujauzito ni kubwa kuliko iliyopatikana kwa kuwa baadhi ya wakuu wa shule walitoa taarifa za uongo na pia baadhi ya familia wamekuwa ‘wakimalizana’ na watuhumiwa bila ya kutoa taarifa.

Amesema awali kabla ya uchunguzi huo walitegemea idadi ya wanafunzi wenye mimba kufikia 100, wakati huo huo amewataka walimu wawaache wanafunzi hao wafanye mitihani yao kwa utulivu na kuwaagiza walimu kuandaa magari ambayo yatasaidia iwapo mwanafunzi yoyote atapata dharura.

Anyika amewataja walimu, waendesha ‘bodaboda’, na wanaume waliooa ni wahusika wa mimba hizo na kuongeza kuwa umaskini ni chanzo kikubwa cha tatizo hilo, na kuwataka wazazi kuwalinda watoto wao na kuwapa elimu juu ya hatari ya mimba za utotoni pamoja na ngono zembe.

 

Tupia Comments