Shirika la utangazaji la Israel liliripoti Jumatano kwamba kumekuwa na ongezeko la kutisha la wanajeshi wanaoiba silaha.
Idhaa ya KAN, yenye uhusiano na Mamlaka ya Utangazaji ya Israel, ilisema kumekuwa na “ongezeko la kutisha la hali ya wizi wa silaha na risasi katika jeshi la Israel chini ya kivuli cha vita huku kukiwa na hofu kwamba wanaweza pia kufikia makundi yenye silaha katika Ukingo wa Magharibi.
” Idhaa hiyo imemnukuu Roi Sharon, mwandishi wa habari wa kijeshi wa idhaa hiyo, akisema “kweli kuna wasiwasi katika jeshi la Israel kuhusu wanajeshi au hata raia kuiba mabomu ya kurusha kwa mkono na makombora ya vifaru kutoka ndani ya Ukanda wa Gaza au maeneo ambayo vikosi vipo.
“Hii inarahisisha mchakato wa askari kuiba maguruneti na makombora ya kukinga vifaru na kuwarudisha nyumbani kama kumbukumbu au kuuza kwa mashirika ya uhalifu,” alisema.