Mtandao wa Wanawake, Katiba, Uongozi, na Uchaguzi ,Katika kuendeleza ajenda ya Katiba yenye mrengo wa jinsia, uliandaa kongamano la kitaifa Mei 20-21, mjini Dar es Salaam ililojumuisha wanamtandao zaidi ya 200 kutafakari na kupanga mikakati ya ushiriki mpana na wenye tija kwa wanawake kuendelea kuongoza harakati za kuchagiza demokrasia shirikishi.
Mtandao huo umebainisha kuendelea kuwepo na vikwazo vingi na vizuizi vingi na upotoshaji wa kudai haki za wanawake hasa kunapokaribia wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi wa Rais mwakani.
Kulingana na uchambuzi yakinifu wa mtandao huo ulibaini mapungufu makubwa katika taratibu na kanuni za uchaguzi ikiwa ni pamoja na uwazi na uchelewashwaji wa hizo kanuni ikiwemo taratibu za uchaguzi wa serikali za mitaa kutofikia wananchi, hali ambayo ina uwezo wa kuchangia kufifisha jitihada za kuelimisha wananchi na kuwaandaa ushiriki wa wanawake katika mchakato wa uchaguzi.
Akisoma tamko mbele ya wahudhuriaji kwenye kongamano hilo kwa niaba ya Mtandao wa WanawakeKatiba Uchaguzi na Uongozi Anna Scholastika Ndagiwe ambaye ni wenyekiti wa shirika la kutetea haki za wanawake, wasichana na watoto mkoani Shinyanga linaloitwa Wanawake LAKI MOJA amesema Wanamtandao wa Wanawake, Katiba, Uongozi na Uchaguzi UNALAANI vikali na KUKEMEA:
‘Kauli za viongozi zinazokinzana aidha kwa makusudi au kwa kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya ajenda ya Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi’.
‘Kauli hizi zinaleta taharuki na kushusha harakati za kudai haki sawa kwa wanawake na wasichana nchini hasa kipindi hiki tunapolekea uchaguzi wa serikali za Mtaa na baadade uchaguzi mkuu hapo mwakani’.
Mwenyekiti Scholastika pia amesema Mtandao wa Wanawake, Katiba, Uongozi, na Uchaguzi pia wanahitaji mambo mbalimbali ya kuzingatiwa ikiwemo :
‘Vyombo vyote vinavyohusika na uchaguzi na usalama wakati wa uchaguzi vitoe mazingira wezeshi, ili wanawake wote waweze kushiriki’.
‘Kadhalika, vyombo vinavyosimamia uchaguzi na utoaji wa haki, viweze kuweka mazingira wezeshi na kusimamia haki katika ngazi zote na ulinzi ‘.
‘Kanuni na taratibu za kuongoza uchaguzi wa serikali za mitaa, uwe wazi, shirikishi na ujumuishe masuala ya jinsia ikiwamo makundi ya watu wenye ulemavu.’
‘Ufuatiliaji wa vikwazo vinavyojitokeza katika ngazi za uchaguzi kwa mfano uteuzi’
‘Vyama vya siasa vihakikishe teuzi za watia nia na wagombea vinazingatia misingi ya usawa wa jinsia na kutoa ulinzi wa kuondoa vikwazo vyote vya ukatili’.
‘Wagombea wote, wakiwamo wa kiume watabeba ajenda inayotetea haki jumuishi ikiwamo za wanawake na Watoto’.