Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Geita imefanya ziara ya kutembelea na kukagua Mradi mkubwa wa Maji ambao unaendelea kutanuliwa maarufu kama Bwawa la Nyankanga ambapo mradi huo unatarajia kukamilika Mwezi Februari mwaka huu .
Akizungumza mara baada ya kukagua Mradi huo unaojengwa kwa thamani ya kiasi cha Shilingi bilioni 1.1 Ndg.Barnabas Mapande ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Geita ameipongeza GEWASA kwa kasi waliyonayo katika mradi huo ambao utawanufaisha wanageita hasa waishio katika wilaya ya hiyo huku akimuomba Mhandisi Frank Chang’awa kukamilisha mradi huo kwa wakati.
“Wakati huo huo tukisubiri zile fedha ambazo Mh. Rais alizitenga kwenye mkoa wa geita ambazo ni Bilioni 24 zitakazo toa maji senga mimi nipongeze gewasa nipongeze gewasa kwa ubunifu huo kwasababu mngelikaa tuu mkasubiri maji yakutoka senga kutarajia kupata mpaka miezi 36 makali yangeendelea kuwa makali, ” Barnabas Mapande.
Mhandisi. Isaack Mgeni ni Meneja Ufundi kutoka Mamlaka ya usafi wa Mazingira Mkoani Geita GEWASA amesema kukamilika kwa mradi huo ni chachu ya wanageita kupata maji safi na salama Huku akisema mradi huo umekamilika mpaka sasa uko asilimia 75 na Mkandarasi anayejenga mradi huo amekwisha kulipwa kiasi cha shilingi Milioni 363.
“Mradi huu kwa upande wa utanuzi wa mtambo wa kutibu maji una shehemu tatu ujenzi wa setensheni una ujenzi wa tenki lakini pia ujenzi wa pampu hausi pamoja na ununuzi wa Pampu Mradi Mh. Mwenyekiti una asilimia 75 tayari Mkandarasi amekwisha lilwa kiasi cha shilingi Milioni 363, “ Mhandisi Isaack.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya siasa ya wilaya kupitia chama cha mapinduzi CCM ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Geita Ndg.Willson Shimo amesema eneo hilo la mradi ni tiba na ufumbuzi mkubwa wa Maji katika maeneo ya Mjini huku akitoa rai kwa mkandarasi anayejenga mradi huo kwa kuupanua kuhakikisha anakamilisha kwa wakati.