Baada ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso kutoa mwezi mmoja kwa RUWASA Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kuhakikisha Maji yanapatikana katika Kijiji Losinyai kufuatia wananchi kuandamana na kufunga barabara wakidai kupatiwa huduma ya maji,hatimae agizo hilo limetekelezwa na wananchi wameanza kupata huduma hiyo.
Hatua hiyo imekuja Baada ya Ayo TV na Millardayo kuripoti taarifa ya wananchi hao ambao wengi wao wakiwa ni akina mama kuandamana kutokana na changamoto ya kukosekana kwa Maji ya bomba Kijijini
Wakiongea na Ayo TV wananchi wa Losinyai wamesema “Leo tunajisikia furaha sana Kwa kupata Maji maana tumeteseka kwa Miaka mingi,tunatumia mwendo mrefu kutafuta Maji na wakati mwingine tunalala huko nje,tunapata maumivu sana kunyanyua ndoo za Maji kwenye magari makubwa sisi ndio tuliandamana kwa kukosa Maji,ila sasa hatutaandamana tena tunaomba Rais atusamehe hatutaandamana tena”
Mwenyekiti wa Kitongoji Benedict John ambapo mradi huo wa Maji umeanza kutekelezwa amesema “Kabla ya hapa wananchi wangu walikuwa wanateseka,walikuwa wanaenda kuchukua Maji Arusha,Moshono huko wengine wanalala uko wanakuja siku ya pili, wengine wanaumia kwenye magari ya michanga,lakini kwa Leo tunamshukuru Mungu kweli Mama ameongea na akatekeleza jambo ambalo limetufurahisha Kwa kweli Leo ni siku ya tatu tukacheka na kufurahi na tunatamani kufanya Party kubwa sana hapa tuchinje Ng’ombe kwaajili ya kumshukuru Mama yetu ”
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Fakii Lulandala amesema mpango wa kupata Maji ni mpango endelevu tangu serikali ya Rais Samia ilipoingia madarakani kuhakikisha anamutua Mama ndio kichwani ,anatamani kuona Kila mwananchi anaunganisha Maji nyumbani kwake na Maji hayo kupatikana kwa bei rahisi
Nae Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Simanjiro Mhandisi Joanes Martin amesema Baada ya maji kufikishwa hapo yanaanza kusambazwa katika Maeneo mengine ambapo Zaidi ya wananchi elfu nne wanakwenda kunufaika huku akiwaomba wananchi kulinda miundombinu hiyo ambayo imepitishwa katika maeneo yao ili miradi hiyo iweze kuwa endelevu