Mwenge wa Uhuru 2024, umekagua na kuzindua kituo cha afya Budushi kilichopo kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza ambacho kimegharibu zaidi ya shilingi milioni 665.4.
Imeelezwa Wananchi wa eneo hilo walijitolea hekari 7 zenye thamani ya zaidi ya Milioni nane, huku Halmashauri ya wilaya ya Kwimba ikichangia milioni mia tatu ikiwa ni mapato yake ya ndani, huku kiasi cha milioni 356, kutolewa na TASAF.
Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Kwimba umekimbizwa zaidi ya kilomita 35, ukizindua jumla ya miradi sita ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na mradi wa maji kijiji cha Mhulya, upandaji wa miti ya matunda shule ya sekondari Walla, uzinduzi wa vyumba kumi vya madarasa na ofisi 4, ufunguzi wa barabara ya lami sokoni – Das House km 1.36, pamoja na kutembelea kituo cha watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi Kakoli.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kwimba Ng’wilabuzu Ludigija amethibitisha kuupokea Mwenge huo wa Uhuru na kuahidi kuulinda na kuwalinda wakimbiza Mwenge kipindi chote wawapo wilayani humo.