Wananchi halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi mkuu wa Rais,madiwani na wabunge unaotarajiwa kufanyia mwishoni mwa mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na afisa mwandikishaji Jimbo la Morogoro Mjini Faraja Maduhu wakati akifungua mafunzo ya maafisa waadikishaji wasaidizi ngazi ya kata Jimbo hilo
Amesema Jimbo la Morogoro Mjini litakuwa na vituo 313 vitatumika kwa zoezi la uandikishaji daftari la kudumu la Mpiga kura Ili kurahisisha zoezi hilo.
Amesema ili kuwepo na viongozi imara na wenye sifa ni muhimu wananchi wakawa sehemu ya kufanya maamuzi ya kuchagua wanaowataka lakini ili hayo yote yatokee ni muhimu wananchi wakajitokeza katika zoezi ili la uandikishaji wapiga kura wakajitokeza kwa wingi.
Aidha amewataka wanashirikiana na mawakala wa vyama vya siasa vyote ili zoezi hilo la uandikishaji liweze kukamilika kwa wakati.
Juma Mpule ni mkazi wa Morogoro amesema Zoezi hilo ni muhimu Kwani linatoa fursa Kwa wananchi kuchagua viongozi wanaowapenda.
Amesema waache kusikiliza baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakihamasisha wananchi kutojitokeza katika Zoezi hilo kwani hawana nia njema.
Zoezi la kuboresha taarifa za mpuga kura daftari la kudumu linatarajiwa kuanza machi 1_ hadi machi 7 mwaka huu Mkoani Morogoro na baadhi ya maeneo mengine nchini.