Zaidi ya wanachi mia mbili wilayani Uyui waliotoa maeneo yao kupisha ujenzi wa umeme Gridi ya Taifa wameiomba serikali kuwalipa fidia ya maeneo hayo kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 500 kwa kuwa kwasasa wamekosa maeneo mbadala ya kufanya shughuli zao za kuwaingizia kipato.
Wananchi hao wametoa malalamiko hayo wakati zoezi la kuwasha wa meme katika kijiji cha Katunda wilayani Uyui ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa mradi wa umeme katika vijiji 61 vilivyopo wilayani hapo kupitia wakala wa nishati vijijini (REA).
Akijibu changamoto ya wananchi kutoa maeneo yao kupisha ujenzi wa miondombinu ya umeme bila kulipwa fidia Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema selikari mejipanga kufia mwezi Oktoba,2023 italipa fidia zote za wanachi walio pitiwa na mradi.