Makamu Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi, Jaji(R) (MST) Mbarouk S. Mbarouk amewataka Watanzania kutojiandikisha jina lake zaidi ya mara moja katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura huku akieleza kuwa endapo likitokea suala kama hili hatua za kisheria zitatumika ili kuhakikisha kuna kuwa na haki na uadilifu katika uchaguzi.
Makamu Mwenyekiti Mbarouk ameyaeleza wakati akifungua mkutano wa tume na Wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mhe. Mbarouk amesema kwamba zoezi la kujiandikisha mpiga kura linapaswa kufanyika kwa uangalifu na kwa kuzingatia
sheria zilizopo.
“Ni kosa kubwa kisheria kwa mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja endapo ikitokea hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi ya
watakaoshirikiana katika vitendo hivyo na Ikumbukwe kuwa uchaguzi ni mchakato wa haki na tutahakikisha kuwa hakuna mtu atakayekosa haki ya kupiga kura wala mtu yeyote atakayejihusisha na udanganyifu”, amesema Mbarouk
Hata hivyo zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaendeshwa na kauli mbiu inayosema ” Kujiandikishia kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora”.