Wananchi wa Mtaa wa mshikamano, kata ya Mbezi wilaya Ubungo wametishia kuandamana kwa shinikizo la kukosa maji kwa muda mrefu
Mara baada ya kufika eneo hilo Afisa mteandaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire akizungumza na wananchi hao ameeleza kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) inaendelea na mchakato wa manunuzi ya pampu zitakazosaidia kuongeza ufanisi katika mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Juu ambao husambaza maji katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Mbezi katika Wilaya ya Ubungo.
“Tunatambua eneo la Mshikamano ni moja ya maeneo yenye changamoto ya upatikanaji maji ambayo DAWASA tunalazimika kuyapatia maji kwa awamu, Kama DAWASA tunaahidi kufikisha maji kwa Wananchi kwa siku tulizokubaliana ili kupunguza changamoto za kihuduma” Mhandisi Bwire