Wananchi wa Kata ya Mkomazi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga wamemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo, Jokate Mwegelo kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya Tembo ambao wamekua wakiharibu mazao yao.
Wakiongea katika mkutano wa hadhara Wananchi ambao wengine walionesha hisia zao hadi kupelekea kulia mbele ya DC, wamesema kuwa wamekuwa wakipitia kipindi kigumu kutokana na Tembo hao kuharibu mazao yao mara kwa mara .
Sakina Abdallah ambaye ni mmoja wa Wananchi wanaopitia changamoto hiyo amesema anapitia wakati mgumu sana kutokana ana Tembo hao kuharibu mazao yake “Kwakweli Mama napitia wakati mgumu sana naomba nisaidie naishi pembezoni huko ndo kila siku Tembo wamekuwa wakituathiri tusaidieni jamani Tembo ana haki na sisi tuna haki tunaomba tusaidiwe kwakweli “
Aidha Mara baadaya ya kusikiliza kilio cha Wananchi DC Jokate Mwegelo ametoa maelekezo kwa Mamlaka ya Wasimamizi wa Wanyamapori (TAWA) kubaki eneo hilo kwa kipindi cha mwezi mmoja ili Wananchi hao waendele na za kilimo hadi watakapovuna, pia ameagiza Vijana wa eneo hilo wapewe mafunzo na vifaa ya kukabiliana na Tembo.