Wanawake 13 kutoka Ufilipino wamehukumiwa kifungo cha miaka minne jela na Mahakama ya Mkoa wa Kandal Nchini Cambodia baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya kubeba mimba kwa lengo la kuuza Watoto kwa Watu wengine.
Mahakama ilisema ushahidi ulionesha wazi kwamba Wanawake hao walikusudia kubeba ujauzito na kuwauza Watoto hao kwa malipo baada ya kujifungua jambo ambalo ni kinyume na sheria za Cambodia, Ingawa hawatafungwa mpaka wajifungue haikuelezwa Watoto hao watapewa hatima gani baada ya kuzaliwa.
Aidha Polisi wa Cambodia walikamata Wanawake hao wakati wa msako kwenye Nyumba moja karibu na Mji mkuu wa Phnom Penh mnamo Septemba 23 kabla ya Maofisa kutoka Ufilipino kusema Wanawake hao ni waathirika wa usafirishaji haramu wa Binadamu hata hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cambodia Chou Bun Eng alikanusha hilo na kudai kwamba Wanawake hao walihusika moja kwa moja na walijua walichokuwa wakifanya.
Kesi hiyo imeibua mjadala mkubwa kuhusu biashara ya kubeba mimba kwa malipo ambayo imekua ikishamiri Nchini Cambodia licha ya kupigwa marufuku biashara hiyo imeendelea kinyemela na hasa kwa Wanandoa kutoka China wamekuwa Wateja wakunwa sana wa biashara hiyo ambao wanaripotiwa kulipa kati ya dola 40,000 (sawa na takribanj shilingi milioni 100 za kitanzania) na dola 100,000 (sawa na takribani shilingi milioni 250 za kitanzania) kwa huduma hizo.
Pia imeripotiwa Mwanamke mmoja wa Cambodia aliyesaidia kundi hilo kwa kuwahudumia chakula alihukumiwa kifungo cha miezi miwili huku Wanawake wengine kutoka Vietnam na Ufilipino ambao hawakuwa Wajawazito wakirudishwa Nchini mwao baada ya kukamatwa.