Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amechangia kiasi Cha shilingi Mil.10 kwa wajasiriamali wadogowadogo 600 waliopatiwa mafunzo maalum yanayoratibiwa na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Tanga Mhe.Husna Sekiboko.
Akizungumza mara baada ya kuchangia Mil.10 Mhe.Aweso amesema kuwa hawezi kuwasahau waliomtoa.
“Dada Husna umenikumbusha 2015 Wakati nimemamliza masomo yangu ya chuo na kusema Marekani yangu ni Pangani nakutangaza nia ya kugombea ubunge nilikataliwa na watu wengi lakini wamama walinikubali na kuniheshimisha na Mimi nawaheshimisha Kwa kutoa kiasi Cha shilingi Mil 10 kwenu”
Naye Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Mhe.Husna Sekiboko amesema kuwa “natekeleza maagizo ya Kamati Kuu ya CCM ambayo imedhamiria kutoa mafunzo kwa wanawake wajasiliamali pamoja na wa UWT Ili kuwapa mbinu za kujikwamua kiuchumi na pia
niwejiwekea utaratibu wa kutembelea tarafa kwa tarafa na nimefanya hilo Kwa tarafa zote za Mkoa wa Tanga ambapo nimesikiliza kero mbalimbali za wananchi na pia kukutana na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa matenki ya Maji lakini pia kuchangia ujenzi wa zahanati katika shule na kuzitatua peke yangu nyingne nliwasilisha kwenye Chama na Kwa ushauri na kutatuliwa.
Katika ziara zake Mhe. Sekiboko amesema kuwa sehemu kubwa ya changamoto ni mikopo ya wajasiliamali wadogowadogo ambapo walikuwa wanahitaji Elimu juu ya uendeshaji wa biashara hiyo ambapo nimejitahidi kuleta mafunzo hayo maalum kwa ajili ya kujifunza na wakitoka hapa wakawafundishe wanawake wengine, pia amegawa mitungi ya gesi ya nishati safi 600 kwa kuwafundisha akina mama juu ya matumizi ya nishati safi huku mitungi mingine 400 akiendelea kutoa katika Wilaya nyingine Ili kutunza mazingira yetu.
Aidha Mhe.Sekiboko ameongeza kwa kusema kuwa katika kutoa Elimu unyanyasaji wa kijinsia ni tatizo katika Jamii yetu na kuwasihi kina mama kujikita katika malezi ya watoto na kukemea vitendo viovu.