Wakati wa kuadhimisha miaka 15 ya Taasisi ya ULINGO na miaka 30 ya Azimio la Beijing imetajwa kuwa hivi sasa ni wakati muafaka kwa wanawake waliokaa muda mrefu kupitia Viti Maalum Bungeni kuwaachia nafasi vijana ili kuendeleza harakati za uwezeshaji wa wanawake katika siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwenye kongamano hilo Sophia Simba ameeleza kuwa Taasisi ya ULINGO, ambayo imefikisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwake, imekuwa chachu kubwa ya kuwainua wanawake katika siasa bila kujali vyama vyao hivyo ni wakati sasa wao kuwaachia vijana chipukizi na wenye nguvu kulitumikia taifa katika nyadifa mbali mbali
“ULINGO imekuwa na mafanikio makubwa. Tumeona wanawake wengi wakiwa wabunge, madiwani na hata vijijini akina mama wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali,”