AyoTV

PICHA 6: Uwanja ambao Serengeti Boys wanaweza kuweka historia leo

By

on

Timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kesho May 21 2017 itacheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi B wa kuwania nafasi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya AFCON U-17 dhidi ya Niger katika uwanja wa Port Gentil uliyopo katika kisiwa cha Port Gentil.

Serengeti Boys watacheza katika uwanja huu ambao ulitumika katika michezo ya fainali za AFCON za wakubwa walizocheza mwezi January mwaka huu, hivyo watahitaji sare au ushindi ili wafuzu kucheza nusu fainali ya , uwanja huo ulijengwa 2015 na unauwezo wa kuchukua mashabiki 20000.

Serengeti Boys leo watacheza uwanja huu wa Port Gentil na kama watashinda au kupata sare ya aina yoyote ile wataweka rekodi ya kushiriki na kuingia nusu fainali ya michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza katika historia, hivyo watapata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la vijana moja kwa moja kufuatia matokeo hayo, michuano ambayo itachezwa India mwishoni mwa mwaka huu.

VIDEO: Tazama hapa chini mazoezi ya Serengeti Boys wakiwa Gabon

Soma na hizi

Tupia Comments