Michezo

Saa kadhaa kabla ya dirisha la usajili kufungwa Southampton yaweka kikao na Mkenya huyu…

on

Klabu ya Southampton ya Uingereza bado inahangaika namna ya kumzuia kiungo wa kimataifa wa Kenya anayeichezea klabu hiyo Victor Wanyama asiihame Southampton, kupitia mtandao maarufu wa habari za michezo wa goal.com umeeleza namna ya viongozi wa klabu hiyo walivyo kaa kikao na Wanyama na wakala wake ili asihame.

victorwanyama_getty150115

Wanyama ambaye siku ya August 28 aliomba uongozi wa Southampton umuuze, hakuwa sehemu ya timu iliyoshinda goli 3-0 dhidi ya Norwich, kocha wake Ronald Koeman alisema Wanyama hakucheza mechi hiyo kwa sababu hakuwa fit kiakili na kimwili hivyo isingekuwa rahisi kwake kumpanga.

Victor-Wanyama-scores-for-014

Kiungo huyo wa Kenya ambaye amebakiza mkataba wa miaka miwili klabuni hapo toka pale alipojiunga mwaka 2013 akitokea klabu ya Celtic ya Scotland, anahusishwa kuhamia katika klabu ya Tottenham Hotspur, sasa bado haijajulikana kama klabu hiyo itamruhusu ahame katika dakika za mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments