Wafungwa 15 wa Kipalestina walioachiliwa kutoka jela za Israel kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa kati ya Hamas na Israel, watawasili Uturuki hii leo, wakitokea mji mkuu wa Misri, Cairo, Quds Press iliripoti.
Takriban Wapalestina 99 walioachiwa huru waliwasili Misri jana kama sehemu ya makubaliano hayo.
Chanzo cha habari katika harakati ya Hamas kiliiambia Quds Press kwamba Turkiye, Qatar, Pakistan, na Malaysia zimekubali kuwakaribisha Wapalestina walioachiliwa huru huku mawasiliano yakiendelea na Algeria na Indonesia kuwakubali wengine.
Chanzo hicho kilisema Tunisia ilikataa kuwakaribisha Wapalestina, ikibaini kwamba Misri, kituo cha kupita, imekubali kuwahifadhi wafungwa ambao ni wa vuguvugu la Fatah pekee.
Misri imetenga hoteli inayomilikiwa na jeshi katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala kuwakaribisha Wapalestina walioachiliwa huru. Hamas imetilia shaka gharama kubwa za hoteli hiyo, hata hivyo Qatar iliahidi kulipia gharama hizo.