Wajumbe wa Israel na Hamas waliondoka katika mji mkuu wa Misri, Cairo, Jumapili mchana, kufuatia mkutano na wapatanishi wa Misri na Qatar katika duru ya hivi punde ya mazungumzo yenye lengo la kuhitimisha usitishaji vita unaoendelea Gaza, vyanzo vya habari viliripoti.
Kwa kukosekana kwa makubaliano ya mwisho wapatanishi, iliripotiwa, walipendekeza makubaliano ya sehemu kwa wakati huu, na kukamilika kwa hatua zilizobaki baadaye.
Shirika la habari la Reuters limenukuu vyanzo viwili vya usalama vya Misri vikisema kuwa mazungumzo hayo yamemalizika bila ya makubaliano na si Hamas wala Israel kukubaliana na mapatano yaliyopendekezwa na wapatanishi.
Mambo muhimu ya kuzingatia katika mazungumzo hayo ni pamoja na kuwepo kwa Israel katika Ukanda wa Philadelphi, eneo nyembamba la urefu wa kilomita 14.5 (maili 9) kando ya mpaka wa kusini wa Gaza na Misri au kuahidi usitishaji vita wa mwisho. Hamas kimsingi inakataa kukubali masuala yote mawili.
Ujumbe wa Israel umeripotiwa kupendekeza kupeleka tena vikosi vyake ndani ya Ukanda huo, huku wakidumisha uwepo wa kudumu katika vituo 12 vya kupelekwa, vingi vikiwa kaskazini mwa Ukanda huo, pamoja na mhimili wa Netzarim.