Habari za Mastaa

Warembo TXC kutua Tanzania, kunogesha ‘Arusha na DAR’ wikiendi hii

on

Good news ninayotaka kukusogezea kwa wewe mpenda burudani hususani muziki wa Afrika Kusini maarufu kama Amapiano ni kwamba warembo wanaounda kundi la liitwalo  TXC akiwemo  Tarryn & Clair wanatarajiwa kutua katika ardhi ya Samia wikiendi hii.

Tarryn na Clair

Tarryn na Clair utakuwa ni ujio wao wa mara ya kwanza kuja Afrika Mashariki kuonesha vipaji vyao vya kuzichesha nyimbo  zinazotamba kwasasa almaarufu kama Amapiano, wakali hao wanatarajiwa kuwasili wiki hii  nchini Tanzania wakitokea Afrika Kusini na kutoa burudani ijumaa tarehe 11th mkoani Arusha katika chimbo liitwalo Le Patio na Jumamosi hii tarehe 12th wataendeleza mwendelezo wa burudani zao ambapo itakuwa ni zamu ya wana Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mmiliki wa kampuni ya Str8upvibes aitwae Sniper Mantana alisema ‘Tunachotaka kuona mashabiki wanapata ladhaa tofauti tofauti miaka kadhaa watu wetu wamezoea kuona tunawaleta Wanaija na wenginro lakini kwasasa tunachanganya ladhaa tofauti na ningependa kusema mwaka huu kuna  vitu vingi vizuri, mashabiki wajiandae’– Sniper Mantana

Kuhusu Tarryn na Clair wanakuja wikiendi hii kutoa burudani Tanzania ni Ma DJ’s wazuri nimeshuhudia shows zao kupitia mitandaoni ninaamini na wameniahidi kufanya makubwa tarehe 11th mkoa wa arusha na tarehe 12th watatoa burudani Dar es Salaam’- Sniper Mantana

UNAWEZA UKATAZAMA HAPA TXC WALIVYOTOA BURUDANI YA DAKIKA 50 KATIKA SESSION IITWAYO AVENUE

 

 

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments