Burudani

Wasanii 9 Tanzania watakaopewa tuzo kwa kusikilizwa zaidi 2021

on

Jumla ya wasanii tisa wa Bongofleva  watapokea tuzo wiki hii kwa kuvunja rekodi ya kuwa na wasikilizaji wengi  Boomplay.

Tuzo hizo almaarufu ‘Boomplay Plaques’ hutolewa mara moja kila mwaka ili kutambua jitihada za wasanii wanaofanya vizuri kwenye App ya Boomplay.

Hii ni mara ya pili kwa tuzo hizo kutolewa ambazo ni mahususi kwa wasanii ambao wameendelea kufanya vizuri kupitia kazi zao za muziki ndani ya mwaka mmoja uliopita.

Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli >>> “Wasanii kama Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize, Rayvanny, Nandy, Mbosso, Zuchu, Aslay na Darassa ni baadhi ya wasanii ambao wameendelea kuvunja rekodi kupitia Boomplay ni furaha yetu kuwatambua”

Natasha Stambuli ameongeza kuwa vigezo vilivyotumika kuchagua wasanii ni pamoja na wingi wa usikilizwaji (streams) wa wimbo wa msanii husika, albamu na usikilizwaji unaotokana na ujumla wa nyimbo za msanii. Takwimu za washindi zimechukuliwa kuanzia mwezi Novemba 2020 hadi Mei 2021.

Soma na hizi

Tupia Comments