Katika kukabiliana na changamoto ya Maji nchini, vijana wa Kike takribani 30 wamepewa jukumu la kuwa Malkia wa Maji kwa lengo la kuwa mabalozi watakaokuwa suluhu ya upatikanaji wa maji.
Akizungumza katika hafla iliyowakutanisha vijana hao wa Kike, Mkurugenzi wa TAMWA, Dr.Rose Reuben amesema…“Kuna kazi kwa ajili ya kuwa affect other people hundred and hundreds kupitia wewe ukau affects Umalkia wako wa Maji, kwamba hakika wewe ni Malkia wa Maji, kwa sababu wote tunahitaji maisha mazuri miaka 100 ijayo hatutakuwepo lakini watakaokuwepo watakuwa alama yetu,”.
Naye Jackline Masambila ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, amebainisha kuwa..“Kama mwanafunzi harakati za kutatua changamoto za maji ilianza tangu nipo shuleni na leo nimetimiza moja ya ndoto ambayo nilikuwa nayo kitambo kwa leo hii program ya Malkia wa Maji inahusu wanawake 30 ambao tumewachagua wanaojihusisha na kutatua changamoto mbalimbali za maji, ambapo tumeiandaa kwa muda mrefu tukishirikiana na Vinana Think Tank”
Ndolezi Petrol ambaye ni moja ya waandalizi wa Program ya Malkia wa Maji, amesema…”Kwa sababu ni mwezi wa wanawake, lakini pia tunaona vipindi ambavyo ukame wa maji ukitokea wanawake ndio kundi la waathirika wakubwa wanatumia muda mwingi kutafuta maji,”.
Naye Afisa Miradi wa Think Tank, Mansusa Kingu amesema “Ni mfumo ambao umechagua na kuangazia masuala ya maji na upatikanaji wake nchini Tanzania ambao unawakutanisha wanawake watakaoenda kutatua changamoto katika miji yetu ikiwemo Dar es Salaam na watakuwa mabalozi wa maji,”.